KATIKA KUHAKIKISHA JUHUDI ZA RAHISI SASA COMPANY YA SMILE WE-CARE IMEKUJA KWA KUHAKIKISHA TANZANIA YA VIWANDA
Na Doreen Aloyce ,Dodoma
KATIKA kuhakikisha juhudi za Mh.Rais John Magufuli ya Serikali ya viwanda zinaendelea ,Kampuni ya Smile we care inayojihusisha kukwamua watanzania kuwa na mafanikio kupitia ujuzi mbalimbali kwa kutengeneza bidhaa za biashara watu zaidi ya elfu tano nchini Tanzania wamenufaika na mafunzo hayo ambayo wamekuwa wakiyatoa.
Hayo yalieelezwa jana na Msemaji wa Kampuni hiyo jijini Dodoma, Jane Mwenda wakati walipokuwa kwenye sherehe ya kuadhimisha mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwa kampuni hiyo yenye makao makuu jijini Dar es salaam ambayo ilienda sambamba na mafunzo ya utengenezaji wa sabuni,keki na bidhaa nyingine.
Jane alisema maadhimisho hayo yamewakutanisha vijana zaidi ya 100 kutoka mikoa mbalimbali Tanzania ambao kupitia mafunzo hayo yamekuwa tiija katika kuleta maendeleo hapa nchini na kwamba kampuni hiyo ilitokea nchini Naigelia.
Alisema kampuni hiyo ilianzishwa kwa lengo la kuhakikisha wanamuunga mkono Rais John Magufuli kuwainua watanzania kutoka hali ya chini mpaka kufikia malengo huku wakianzisha viwanda vidogo vya ujasiliamali ambapo tangu imeanzishwa mwaka jana zaidi ya watanzania elfu 5000 tayari wamenufaika kupitia mafunzo ambayo wamekuwa wakipewa.
"Yapo makampuni ya kitapeli ambayo lengo lao ni kutapeli watanzania,ila sisi tumejikita kuinua uchumi wa watanzania wakiwemo vijana na watu wazima ambapo wanachangia kiingilio cha elfu ishirini na tatu tu wataweza kuwafundisha utengenezaji wa sabuni,batiki,keki, shampuu,mafuta ya kupaka, mishumaa, na vitu vingi lengo nikuwasaidia kupambana na hali ya maisha kukuza uchumi wao na leo tutawazawadia waliofanya vizuri "
"Kupitia mafunzo haya inasaidia kutatua changamoto mbalimbali kwa vijana hususani kuondoa wizi mitaani,kuondoa ombaomba ,ukaaji wa vijiweni na wengine kutojingiza kwenye makundi ya kuwaangamiza na badala yake watakuwa wametingwa na ujasiliamali "alisema Mwenda.
Aliiomba serikali kuangalia namna ya kuwaunga mkono kutoa nafasi zaidi kutoa elimu kwa vijana ili waweze kuwafikia vijana wengi na hatimaye faida kwa watanzania wote.
Nae Erick Malek maalufu kama Dkt. Kodak kutoka Jijini Dar es salaam ambaye ni mshauri wa Kampuni hiyo alisema kuwa vijana wengi wanazunguka mtaani bila kujua mwelekeo na kudai kwamba vijana watambue kuwa maisha ni maamuzi wasikate tamaa ili kutimiza ndoto ya maisha yao kuwa wanapaswa kujitoa ili Mungu aweze kubariki kazi zao huku akiwasihi kutojihusisha na makundi ambayo hayana tija.
Taji Julius ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma (Udom) alisema kampuni hiyo imekuwa fursa kwake kwani amepata faida kubwa katika kujikimu kwenye mahitaji madogo pale anapotengeneza bidhaa ndogondogo kutokana na kutopata mkopo wa serikali hivyo kupelekea kutatua changamoto zinazomkabili.
Alisema kuwa vijana hususani wana vyuo wanayo fursa ya kutumia mitandao ya kijamii kwa mambo yenye manufaaa badala ya kutumia kwa ajili ya mambo ambayo hayana tija na kwamba pale wanapohitimu vyuo tayari watakuwa na ajira binafsi kupitia ujasiliamali.
Mwisho kazi njema.










































































































Maoni
Chapisha Maoni